Home Biashara Safaricom kuongeza ada za utoaji huduma

Safaricom kuongeza ada za utoaji huduma

Kulingana na Safaricom miongoni mwa huduma zitakazoongezwa ada ni kupiga simu,kutuma arafa,data,fibre na M-pesa ambayo itaongezwa kati ya asilimia 12 na 15.

0

Kampuni ya kutoa huduma za mawasiliano nchini,Safaricom imetangaza kuongeza ada kwa huduma zake zote kufuatia kutekelezwa kwa sheria za fedha za mwaka 2023.

Safaricom imetoa tangazo hilo Jumamosi ,siku moja baada ya mahakama ya rufani kuondoa marufuku iliyowekwa ya kutekelezwa kwa sheria hizo mpya za fedha zinazopendekeza matozo kadhaa mapya.

Kulingana na Safaricom miongoni mwa huduma zitakazoongezwa ada ni kupiga simu,kutuma arafa,data,fibre na M-pesa ambayo itaongezwa kati ya asilimia 12 na 15.

Website | + posts