Home Biashara Safaricom kufanyia mfumo wa M-Pesa ukarabati Jumatatu

Safaricom kufanyia mfumo wa M-Pesa ukarabati Jumatatu

0
kra

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imetangaza kuwa itafanyia ukarabati mfumo wa kutuma pesa kwa njia ya rununu M-Pesa siku ya Jumatatu.

Kupitia kwa taarifa katika mtandao wake wa X leo Jumamosi, kampuni hiyo ilisema ukarabati huo utafanywa kati ya saa saba na saa saba na nusu usiku.

kra

“Kama sehemu ya uboreshaji, tutafanyia mfumo wetu ukarabati Jumatatu, Juni 24, 2024 kunzia saa saba hadi saa saba na nusu usiku,” ilisema taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa hiyo, wateja hawataweza kupata huduma zote za M-Pesa wakati wa kipindi hicho cha ukarabati.

Hata hivyo, kampuni hiyo ilisema huduma zingine ikiwa ni pamoja na kupiga simu, jumbe fupi na data zitapatikana.

Kampuni hiyo imewaomba radhi wateja wake watakaotatizika na shughuli hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here