Home Habari Kuu Ruto: Serikali kukodisha bandari ya Mombasa

Ruto: Serikali kukodisha bandari ya Mombasa

0

Rais William Ruto amesema serikali itakodisha bandari ya Mombasa kwa wawekezaji wa kibinafsi ili kuboresha utoaji huduma na kubuni nafasi zaidi za ajira.

Ruto aliyasema haya siku ya Juampili katika eneo la Mama Ngina Water Front.

Ras alisisitiza kuwa ni kupitia tu kwa kukodishwa kwa bandari ambapo huduma zitaboreshwa na kuifanya bandarai ya Kenya kuwa miongoni mwa bandari bora barani Afrika.

Hata hivyo, Rais alikanusha madai ya kubinafsishwa kwa bandari ya Mombasa, akiongeza kuwa wakodishaji watairejesha baada ya muda wao kukamilika.

Website | + posts