Home Habari Kuu Ruto: Kesi za ufisadi za mabwawa ya Aror na Kimwarer zilichochewa kisiasa

Ruto: Kesi za ufisadi za mabwawa ya Aror na Kimwarer zilichochewa kisiasa

0

Rais William Ruto amesema kesi ya ufisadi iliyowasilishwa mahakamani na serikali iliyopita katika ujenzi wa mabwawa ya Aror na Kimwarer, ilikuwa ni njama ya kisiasa dhidi ya washtakiwa.

Ruto akijibu maswali kutoka kwa wanahabari siku ya Jumapili amesema kesi hizo ziliporomoka kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Ruto amekariri kuwa hakuna yeyote atakayesazwa katika kesi dhidi ya ufisadi na kuwaonya wahusika kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Website | + posts