Home Habari Kuu Ruto: Uwezo wa kawi safi haujakua Afrika

Ruto: Uwezo wa kawi safi haujakua Afrika

0

Rais William Ruto amesema kwamba uwezo wa kawi safi uliongezeka kwa kiwango kikubwa ulimwenguni mwaka 2023 ambapo gigawatt 500 ziliongezwa na uwekezaji wa dola bilioni 600.

Hata hivyo, kiongozi wa nchi alilalamika kwamba bara Afrika liliongeza gigawatt tatu pekee mwaka huo, ilhali bara hili linatoa fursa nyingi za kawi safi kwa wawekezaji wa kaskazini kwa matokeo yenye manufaa kwa wote.

Kiongozi wa nchi aliyasema hayo alipohutubia mkutano kuhusu biashara ya ushughulikiaji wa mabadiliko ya tabianchi na mpito hadi kawi isiyokuwa na kaboni mjini Seoul nchini South Korea.

Rais Ruto anahudhuria kongamano la Korea na Afrika ambalo alisema kwamba linatoa fursa ya kuboresha uhusiano wa kidiplomasia na kutumia uwezo wa nchi hizi mbili kuhakikisha ukuaji wa pamoja, kushughulikia changamoto za ulimwengu na kuimarisha mshikamano kwa ajili ya amani na usalama.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here