Home Habari Kuu Ruto: Tunapaswa kusawazisha matumizi ya kawaida na maendeleo

Ruto: Tunapaswa kusawazisha matumizi ya kawaida na maendeleo

0

Seikali inadhamiria kutafuta usawazishaji mwafaka kati ya matumizi ya fedha za maendeleo na yale ya kawaida.

Rais William Ruto amesema serikali inatumia rasilimali nyingi kwa matumizi ya kawaida kuliko kiwango kinachohitajika.

Alisema takriban asilimia 46 ya matumizi ya fedha za nchi yanaenda kwa mishahara na ujira.

“Hii ni juu zaidi ya lengo letu la asilimia 35. Tunapaswa kupunguza kiwango hicho,” alisema Rais Ruto akiongeza kuwa hatua hiyo itahakikisha mpango wa maendeleo ya nchi haukwami kutokana na uhaba wa fedha.”

Alitoa kauli hizo leo Jumanne katika Ikulu ya Nairobi, wakati wa kuapishwa kwa Makatibu Salome Muhia-Beacco wa Huduma za Magereza na Anne Wang’ombe wa Utendakazi na Utoaji Huduma.

Rais aliwataka wawili hao kufanya kazi na mawaziri wao kutimiza ajenda ya serikali.

“Wakenya wanatarajia sisi kutimiza ahadi zetu na kuboresha maisha yao. Mna uelewa unaohitajika kutimiza ajenda hii.”

Aliitaka Idara ya Utendakazi na Utoaji Huduma kuhakikisha watumishi wa umma wanawajibishwa, kuboresha utendakazi wao na kulipwa mishahara bora ipasavyo.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here