Rais William Ruto leo Alhamisi katika Ikulu ya Nairobi anatarajiwa kuongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri kuangazia masuala mbalimbali yenye umuhimu kwa taifa.
Mkutano huo utakuwa wa kwanza tangu kuzuka kwa maandamano ya vijana wiki mbili zilizopita.
Wakati wa mkutano huo, maswala yaliyoibuliwa katika maandamano ya vijana wa Gen Z yanatarajiwa kupatiwa kipaumbele.
Maswala hayo ni pamoja na kumtaka Rais awatimue mafisadi serikalini, kutafuta suluhu kwa changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana na kupunguza matumizi ya serikali.