Rais William Ruto anatarajiwa kusafiri kuondoka Jumapili jioni kuelekea Beijing,China kuhudhuria kongamano la tisa la ushirikiano kati ya mataifa ya Afrika na China(FOCAC).
Kongamano hilo litaandaliwa baina ya tarehe 4 na 6 mwezi huu na linashirikisha mataifa yote ya Afrika isipokuwa Eswatini.
Akiwa nchini china Ruto anatarajiwa kufanya mikutano kadhaa na viongozi wa mataifa yatakayohudhuria kongamano hilo, kuimarisha ushirikiano wa Kenya kimataifa.
Itakuwa ziara ya kwanza ya Ruto nje ya nchi tangu kuzuka kwa maandamano ya vijana wa Gen Z, baada ya kuhudhuria kongamano la Afrika na Korea Kusini mjini Seoul Juni 4 mwaka huu.