Home Taifa Ruto: Kenya Kwanza haijaunda serikali ya muungano na ODM

Ruto: Kenya Kwanza haijaunda serikali ya muungano na ODM

0
kra

Rais William Ruto amebainisha kuwa muungano unaotawala wa Kenya Kwanza haujaunda serikali ya muungano na chama cha ODM. 

Badala yake, Ruto amesema pande hizo mbili zimekubaliana kuliunganisha taifa na kuwahudumia Wakenya.

kra

Akizungumza siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu iliyoanza leo Jumatatu katika kaunti za Kisii na Nyamira, Ruto ameongeza kuwa Kenya Kwanza na ODM zimekubaliana kushikana mikono kwa lengo la kukabiliana na changamoto zinazoikabili nchi.

Alisema hatua hiyo si ya kibinafsi au ya maslahi ya kisiasa bali ilichukuliwa kwa manufaa ya Wakenya wote.

“Wakati huwadia ambapo kitu cha muhimu zaidi si kile kinachowafaidi viongozi au vyama vya kisiasa bali kile kinachowanufaisha watu,” Ruto aliyasema wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Matamshi yake yanakuja wakati ambapo hali ya vuta ni kuvute imeshamiri katika muungano wa upinzani wa Azimio huku chama cha ODM kikilimbikizwa lawama ya kuusaliti muungano huo.

Wanachama wa ODM John Mbadi, Opiyo Wandayi, Hassan Joho na Wycliffe Oparanya wameteuliwa kuwa mawaziri katika serikali ya Kenya Kwanza.

Ni hatua ambayo imevisababisha vyama vya Narc Kenya na PNU kuanza safari ya kuugura muungano huo huku viongozi Kalonzo Musyoka wa Wiper, Eugene Wamalwa wa DAP-K na Jeremiah Kioni wa Jubilee wakiashiria kuunda vuguvugu la kuendelea kutetea maslahi ya Wakenya.

 

Website | + posts