Home Habari Kuu Ruto: Kenya inasimama na watu wa Libya kufuatia mafuriko yaliyosababisha maafa

Ruto: Kenya inasimama na watu wa Libya kufuatia mafuriko yaliyosababisha maafa

0

Rais William Ruto ameelezea kusimama kwa Kenya na watu wa Libya wakati huu ambapo nchi hiyo inakumbwa na mafuriko ambayo yamesababisha maafa. 

Angalau watu 2,300 wamefariki nchini Libya kutokana na mafuriko ambayo pia yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali.

Watu wapatao 10,000 hawajulikani waliko na mamlaka nchini zinahofia idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

“Mshikamano wetu na watu wa Libya kufuatia mafuriko makubwa ambayo yamesababisha vifo na uharibifu wa mali. Kenya inasimama nanyi,” amesema Rais Ruto katika ujumbe wake kwa taifa la Libya.

Jitihada za uokozi zinaendelea wakati mitaa nchini humo ikiwa imefunikwa na vifusi na matope.

Mvua kubwa zilizonyesha nchini Libya zimesababisha mafuriko makubwa ambayo yamesababisha sehemu kubwa ya barabara kufunikwa na maji huku magari yakizama ndani ya maji.

Mvua zilizoshuhudiwa katika maeneo mengi ya mashariki mwa nchi hiyo zilichochea mamlaka kutahadhari, ikiwa ni pamoja na kufunga shule.