Home Biashara Ruto: Kenya iko tayari kwa biashara

Ruto: Kenya iko tayari kwa biashara

0
Rais Ruto akiwa na Waziri Mkuu wa Pakistan Anwaar-ul-Haq Kakar
Rais Ruto akiwa na Waziri Mkuu wa Pakistan Anwaar-ul-Haq Kakar

Kenya iko wazi kwa biashara na ushirikiano utakaowafaidi raia wake.

Hayo yamesemwa na Rais William Ruto wakati wa mkutano kati yake na Waziri Mkuu wa Pakistan Anwaar-ul-Haq Kakar jijini Beijing nchini China anakofanya ziara.

Serikali ya Pakistan imeelezea nia ya kuimarisha ushirikiano wake wa kibiashara na Kenya.

“Tunaunga mkono dhamira ya serikali ya Pakistan kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Kenya kwa kuangazia bidhaa za dawa na vifaa tiba,” alisema Rais Ruto wakati wa mkutano huo.

“Pia tunatizamia kuimarisha uhusiano wetu wa kitamaduuni.”