Home Habari Kuu Ruto azindua ujenzi wa barabara ya Mfangano

Ruto azindua ujenzi wa barabara ya Mfangano

0

Rais William Ruto mapema Jumamosi amezindua ujenzi wa barabara ya Mfangano Island Ring Road iliyoko eneo bunge la Suba kaskazini kaunti ya Homa Bay.

Kwenye ziara hiyo Ruto aliandamana na mwenyeji wake Gavana Gladys Wanga,na mawaziri Kipchumba Murkomen wa uchukuzi na mwenzake wa habari teknolojia na mawasiliano Eliud Owalo.

Ziara ya Rais imeingia siku ya pili Jumamosi ambapo baadae atahudhuria mikutano kadhaa ya kukatana na wananchi.

Ruto yupo kwenye ngome ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kipindi cha siku nne.