Home Kimataifa Ruto ayataka mataifa duniani kukumbatia mabadiliko ya teknolojia

Ruto ayataka mataifa duniani kukumbatia mabadiliko ya teknolojia

0
kra
Rais William Ruto ametoa wito kwa serikali duniani kukumbatia mabadiliko ya teknolojia ili kukuza utendakazi bora na uwajibikaji. 
Amezisihi nchi kutoruhusu uoga wa zisichokijua kuwanyima vijana fursa zinazotokana na teknolojia.
“Ikiwa hatutatumia manufaa yanayotokana na maendeleo tukitumainia usalama, tuko katika hatari ya kupoteza vyote,” alisema Rais Ruto.
Alisema mataifa sharti yasisite kuchukua hatua ya pamoja na kuitekeleza kupitia taasisi ya pande nyingi inayoshughulikia namna binadamu ataendelea katika dunia inayostawi siku zijazo.
Kwa kufanya hili, Rais Ruto alisema mataifa yanaweza yakachangia rasilimali na uelewa wa kuboresha fursa za pamoja za kushinda sasa na katika siku zijazo.
“Kile kinachohitajika ni uwekezaji, unahitaji hatua ya ujasiri na dhamira, kama ile iliyochukuliwa katika uwekezaji uliogeuza majangwa ya Mashariki ya Kati kuwa na maendeleo, kuwa vituo vya siku zijazo kama Dubai,” alisema.
Rais Ruto aliyasema hayo wakati wa mkutano wa viongozi wakuu wa serikali uliofanyika jijini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE.
Hata hivyo, alisema uvumbuzi huchochea upinzani na majaribio ya kuukandamiza au kuukumbatia kwa kuufanya kuwiana na hali ya sasa.
“Uoga wa usichokijua unaweza kuwa halisi na kizuizi cha maendeleo. Hata hivyo, ikiwa serikali zinapaswa kusalia kuwa muhimu, lazima zihamasishe na kukumbatia mabadiliko,” aliongeza Rais Ruto.
Martin Mwanje & PCS
+ posts
kra