Home Habari Kuu Ruto awasili Riyadh kuhudhuria mkutano wa Saudia na Afrika

Ruto awasili Riyadh kuhudhuria mkutano wa Saudia na Afrika

0

Rais William Ruto amewasili jijini Riyadh ambako atahudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa Saudi Arabia na Afrika. 

Mkutano huo ni kwanza kuwahi kuandaliwa.

Mikutano sawia imeandaliwa na nchi za Marekani, China na Urusi, na Saudi Arabia inaonekana kufuata nyayo za nchi hizo zenye nguvu duniani.

Mkutano wa Saudia na Afrika utaandaliwa katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa la King Abdulaziz.

Wakati wa ziara hiyo, Rais Ruto anatarajiwa kutumia fursa hiyo kujadili ununuzi wa mafuta kutoka taifa hilo la Mashariki ya Kati.

Saudi Arabia ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza katika uzalishaji wa mafuta duniani.

Nchini Kenya, bei ya mafuta imekuwa ikiongezeka kila uchao katika hatua ambayo imesababisha kupanda kwa gharama ya maisha.

Serikali inasema imeweka mikakati kabambe inayokusudia kukabiliana na hali hiyo kwa manufaa ya Wakenya wanaolalamikia kuelemewa na mzigo wa kusukuma gurudumu la maisha.