Home Habari Kuu Ruto awasili China kwa ziara ya siku tatu

Ruto awasili China kwa ziara ya siku tatu

0

Rais William Ruto aliwasili jijini Beijing nchini China Jumapili alasiri kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Ruto alilakiwa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping, punde alipotua Beijing.

Katika ziara yake, Ruto anatarajiwa kuhudhuria na kuhutubia kikao cha  kimataifa cha Ukanda Mmoja, Njia Moja maarufu kama Belt and Road Initiative (BRI) kitakachohudhuriwa na viongozi kadhaa wa kimataifa.

Ruto anatarajiwa kuhutubia kikao cha tatu cha mpango wa miundombinu ya barabara cha BRI, ambacho kitaandaliwa mjini Beijing na kuhudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali.

Ruto atahutubia kikao hicho kuzungumzia uchumi wa kidijitali kama chanzo kipya ukuaji.

Rais pia atafanya kikao na mwenyeji wake Rais Xi Jinping na viongozi wengine duniani kuhusu jinsi za kukuza ushirikiano.

Website | + posts