Rais William Ruto ametuzwa tuzo ya mwaka huu ya uwekezaji viwandani unaohimiza matumizi ya nishati safi kupitia kampeni ya mabadiliko ya tabia nchi.
Ruto alipewa tuzo hiyo alipoongoza kikao kisicho cha kawaida cha Marais wa Afrika (CAHOSCC) kuhusu mabadiliko ya tabia nchi pembenzoni mwa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Ruto amesisitiza haja ya kutekeleza makubaliano ya kongamano la COP29 mjini Baku, Azerbaijan mwaka jana, uliopendekeza kuongezwa kwa pesa za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa mataifa ya Afrika.