Home Habari Kuu Ruto asaini Mswada wa Ubinafsishaji, 2023 kuwa sheria

Ruto asaini Mswada wa Ubinafsishaji, 2023 kuwa sheria

0

Rais William Ruto ametia saini Mswada wa Ubinafsishaji, 2023 kuwa sheria.

Unabatilisha Sheria ya Ubinafsishaji, 2025 iliyoidhinishwa kabla ya katiba ya sasa kuanza kutekelezwa mnamo mwaka 2010.

Mswada huo unaondoa urasimu katika ubinafsishaji wa mashirika ya serikali yasiyokuwa ya kimkakati au yasiyotenegeza faida.

Hafla ya utiaji saini mswada huo ilifanyika leo Jumatatu katika Ikulu ya Kisumu na kuhudhuriwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua na Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula.

Wengine waliokuwapo ni Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, Mawaziri Eliud Owalo wa Habari na Mawasiliano na Rebecca Miano wa Biashara na pia kiongozi wa walio wengi katika bunge la Taifa Kimani Ichung’wah.

Mswada huo unahamasisha kushiriki zaidi kwa sekta ya kibinafsi katika uchumi kwa kubadilisha uzalishaji na uwasilishaji wa huduma za umma kupitia kwa mtaji wa kiniafsi na utaalam.

Mswada huo uliowasilishwa na Ichung’wah pia unapendekeza kubuniwa kwa mamlaka ya ubinafisishaji.

Ichung’wah alisema mswada huo unamkabidhi waziri wajibu wa kubuniwa kwa mpango wa ubinafsishaji.

“Mpango wa ubinafsishaji utawasilishwa na kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri. Wajibu wa bunge la Taifa utakuwa kuidhinisha mpango huo,” alielezea Ichung’wah.

 

Website | + posts