Home Biashara Ruto asaini kuwa sheria Mswada wa Matumizi ya Ziada ya Fedha 2024

Ruto asaini kuwa sheria Mswada wa Matumizi ya Ziada ya Fedha 2024

0
kra

Rais William Ruto leo Jumatatu asubuhi ametia saini kuwa sheria Mswada wa Matumizi ya Ziada ya Fedha 2024. 

Ruto alitia saini mswada huo katika Ikulu ya Nairobi wakati wa halfa ambayo ilihudhuriwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua, Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula na Kiongozi wa wengi katika bunge hilo Kimani Ichung’wah miongoni mwa maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini.

kra

Rais amesifia mswada huo akisema utahakikisha kuna fedha zaidi zinazohitajika kufadhili sekta za kilimo, elimu na afya.

Pia utahakikisha utekelezaji wa mpango wa upatikanaji wa afya kwa wote (UHC) kupitia ufadhili wa madaktari wanagenzi, wafanyakazi wa UHC walioajiriwa kwa mikataba na wahudumu wa afya ya jamii.

Mswada huo kadhalika unaunga mkono kuajiriwa kwa walimu wa shule za sekondari za JSS kwa masharti ya kudumu na elimu ya juu kupitia mpango mpya wa ufadhili.