Home Michezo Ruto amwomboleza mwanahabari Cardovillis

Ruto amwomboleza mwanahabari Cardovillis

Pia Cardovillis alikuwa mwanahabari wa michezo katika runinga ya NTV na pia idhaa ya Nation FM.

0

Rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi na wakenya waliojiunga kumwomboleza mwanahabari wa michezo Sean Cardovillis aliyefariki mapema Jumamosi.

Ruto amemtaja marehemu kuwa shupavu na aliyejitolea kutekeleza kazi kwa umakini mkubwa.

Hadi kifo chake marehemu alikuwa mwanahabari wa michezo katika idhaa ya Capital FM na pia mtangazaji aliyebobea katika utangazaji wa mashindano ya mbio za magari.

Pia Cardovillis alikuwa mwanahabari wa michezo katika runinga ya NTV na pia idhaa ya Nation FM.

Cardovillis alipatikana akiwa ameanguka mapema Jumamosi katika vidato vya nyumba yake mtaani Parlands huku uchunguzi kuhusu chanzo cha kifo chake kikichunguzwa na polisi.