Home Habari Kuu Ruto amteua Ingonga Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma

Ruto amteua Ingonga Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma

Ruto amemteua igonga kumrithi Noordin Haji aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi, NIS.

0

Rais William Ruto amemteua Renson Ingonga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma kwa kipindi cha miaka minane.

Ingonga anamrithi Noordin Haji aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu waHhuduma ya Kitaifa ya Ujasusi, NIS.

Hadi uteuzi wake, Ingonga alihudumu kama Naibu Mkurugenzi Mkuu wa afisi hiyo chini ya Haji.

Ingonga ambaye ni wakili katika mahakama kuu ana shahada ya sheria.

Ameteuliwa kupitia kwa gazeti rasmi la serikali la Septemba 20 wiki moja baada ya bunge kumuidhinisha.

Website | + posts