Rais William Ruto anaongoza hafla ya 96 ya tamasha la muziki baina ya shule na taasisi za elimu katika Ikulu ndogo ya Eldoret.
Tamasha hilo linawaleta pamoja wanafunzi kutoka taasisi na shule zilizotawazwa mabingwa wa kitaifa mwaka huu.
Wanafunzi wamepata fursa ya kutumbuiza na kuonyesha umahiri wao katika sanaa ya muziki.
Tamasha hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali nchini akiwemo Naibu Rais Rigathi Gachagua.