Rais William Ruto ameanza ziara ya siku tano eneo la mlima Kenya mapema Jumamosi akitarajiwa kuzuru kaunti za Kiambu, Murang’a, Kirinyaga, na Nyeri .
Ruto ameanza kwa kuzindua mradi wa maji wa Githurai eneo la Ruiru kabla ya kufungua soko la Ruiru.
Mida ya saa tano unusu Rais atasimama Kenol Town mjini Maragua kukutana na wananchi na baadae kufungua mradi wa maji wa Kagio eneo bunge la Ndia saa saba Adhuhuri.
Baadae alasiri Ruto atasimama Karatina kabla ya kufungua barabara ya Marua-Gatung’ang’a-Chieni-State Lodge Road eneo bunge la Mathira .