Rais William Ruto ameagiza jeshi la KDF kutoa ndege za helikopita kusafirisha chakula na dawa kwa waathiriwa wa mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini.
Ruto ameteoa agizo hilo Jumamosi alipoongoza kikako cha dharura kukabiliana na mikasa katika Ikulu ya Nairobi.
Rais amesema kuwa maeneo mengi ya kaskazini mwa nchini yameathirika vibaya na kutengwa kutokana na mafuriko yaliyoletwa na mvua kubwa inayonyesha nchini.
Kikao hicho kilihudhuriwa na maafisa wakuu serikalini wakiwemo mawaziri Kithure Kindiki wa usalama wa taifa ,Aden Duale wa ulinzi na Susan Nakhumicha wa afya.