[contact-form][contact-field label=”Name” type=”name” required=”true” /][contact-field label=”Email” type=”email” required=”true” /][contact-field label=”Website” type=”url” /][contact-field label=”Message” type=”textarea” /][/contact-form]
Ruth Kamande ambaye alihukumiwa kifo na baadaye kubadilishiwa hadi kifungo cha maisha gerezani kwa mauaji ya mpenzi wake mnamo mwaka 2015 ameruhusiwa na Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu dhidi yake katika Mahakama ya Upeo.
Mahakama ya Rufaa inashikilia kwamba Mahakama ya Upeo inastahili kushughulikia haki za wanawake ambao wanadhulumiwa na sera za kisheria za kujikinga wanaposhambuliwa.
Ruth anasemekana kumdunga kisu mara 25 Farid Mohamed Septemba 20, 2015, katika makazi yao mtaani Buruburu kaunti ya Nairobi.
Alipofikishwa mahakamani, Kamande alijitetea akisema alikuwa anajikinga aliposhambuliwa na Farid lakini mahakama haikukubaliana naye.
Rufaa yake ilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa Novemba, 2020.
Yeye ni mmoja wa wafungwa ambao Rais William Ruto alipunguzia hukumu zao kutoka kifo hadi kifungo cha maisha Julai, 2023.
Wakili wa Ruth Prof. Githu Muigai anasema rufaa ya mteja wake inawakilisha suala linalogusa umma wakati ambapo washukiwa wanajitetea kwamba walikuwa tu wanajikinga bila kusudi la kutekeleza mauaji hasa iwapo wahusika walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi.
Majaji Asike Makhandia, Agnes Murgor na Sankale Ole Kantai ndio waliamua kwamba Mahakama ya Upeo ishughulikie suala hilo, ikitizamiwa kwamba visa vya dhuluma za kinyumbani na kijinsia zimeongezeka na wahusika mara nyingi hulazimika kujikinga.