Home Kimataifa Russia yashambulia miundomsingi ya kawi nchini Ukraine

Russia yashambulia miundomsingi ya kawi nchini Ukraine

0
kiico

Jumanne Mei 7, 2024,  usiku, Urusi ilitekeleza shambulizi kali dhidi ya miundomsingi ya kawi nchini Ukraine kwa kurusha makombora na droni zaidi ya 70.

Miundombinu iliyolengwa iko katika jiji la Kyiv na miji mingine sita kulingana na maafisa wa serikali ya Ukraine.

Lengo la Urusi ni kulemaza sekta ya viwanda nchini Ukraine na kuvunja wanajeshi wa nchi hiyo mioyo ili wajiondoe kwenye vita vinavyoendelea.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alikashifu shambulizi hilo ambalo liliathiri pia makazi ya watu na mfumo wa reli katika maeneo kama Lviv, Zaporizhzhia na sehemu za Kusini na Magharibi mwa nchi hiyo.

Watu watatu akiwemo msichana wa umri wa miaka minane waliachwa na majeraha kufuatia shambulizi hilo.

Matokeo mengine ya shambulizi hilo ni ukosefu wa umeme katika maeneo mengi nchini Ukraine huku shirika la umeme likionye kwamba maeneo zaidi ya nchi yatakosa umeme.

Waziri wa kawi nchini Ukraine German Galushchenko alisema kwamba adui hajaacha mipango yake ya kuhakikisha umeme unakosekana nchini humo huku wachambuzi wakisema kwamba lengo ni kuhujumu uundaji wa silaha.

kiico