Home Michezo Rugumayo alenga kuwamotisha wachezagofu wa Uganda

Rugumayo alenga kuwamotisha wachezagofu wa Uganda

0

Ronald Rugumayo ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Uganda na mchezaji pekee aliyesalia kwenye mashindano ya kimataifa ya Magical Kenya Open yanayoendelea katika uwanja wa gofu wa Muthaiga.

Rugumayo aliye na umri wa miaka 32 anasema amefurahishwa na matokeo yake katikamashindano ya mwaka huu na angependa kutumia mashindano hayo kuwatia hamasa wachezaji gofu wa Uganda.

Rugumayo anashiriki mashindano ya Magical Open kwa mara ya nne baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2018 kabla ya kurejea mwaka 2022 na 2023.

Website | + posts