Home Burudani Ruger asema hatashtaki Mkenya anayejisingizia kuwa yeye

Ruger asema hatashtaki Mkenya anayejisingizia kuwa yeye

0
Mwanamuziki Ruger

Mwanamuziki wa Nigeria Ruger amesema kwamba hatachukua hatua yoyote dhidi ya Mkenya anayejiita Ruger wa Kayole.

Katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha redio, mwimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Michael Adebayo Olayinka alisema jamaa huyo wa Kenya anajaribu kujitafutia riziki.

Ruger alisema anamtakia Ruger wa Kayole kila la heri huku akitambua jukumu analotekeleza kuu la kuendeleza muziki wake.

Ruger wa Kayole

“Mwisho wa siku nyimbo ambazo anaimba kwenye tamasha ni zangu sio zake ametunga, baadaye mtu akitaka kupata wimbo huo mitandaoni atarejelea tu kwangu, kwa hivyo ni sawa,” alisema Ruger kwenye mahojiano hayo ya kituo cha BBC.

Ruger ambaye amewahi kutumbuiza kwenye tamasha nchini Kenya zaidi ya mara moja alisihi kila mmoja atulie kuhusu suala la Ruger wa Kayole.

Ruger wa Kayole anamfanana Ruger wa kweli na ana uwezo wa kuimba nyimbo zake kwa ufasaha. Inasemekana huwa anaalikwa kwenye tamasha kuimba nyimbo hizo hapa nchini.

Website | + posts