Home Kimataifa Rosalynn Carter, mke wa Jimmy Carter afariki

Rosalynn Carter, mke wa Jimmy Carter afariki

0

Rosalynn alikuwa mshirika wangu wa karibu katika kila kitu nilichowahi kukifanya, Rais wa zamani Jimmy Carter alisema katika taarifa iliyotolewa na Kituo cha Carter.

Mke wa rais wa zamani Rosalynn Carter, mwanaharakati wa afya ya akili, alifariki dunia akiwa na miaka 96 siku ya Jumapili akiwa nyumbani kwake huko Plains, kwenye jimbo la Georgia, Kituo cha Carter kimesema katika taarifa.

Rais wa zamani Jimmy Carter, mwenye miaka 99, na Rosalynn Carter walikuwa katika ndoa kwa miaka 77. Rosalynn Carter ameacha watoto ambao ni Jack, Chip, Jeff na Amy. Wajukuu 11 na vitukuu 14.

Rosalynn alikuwa mshirika wangu wa karibu katika kila kitu nilichowahi kukifanya, Rais wa zamani Jimmy Carter alisema katika taarifa iliyotolewa na Kituo cha Carter. Alinipa mwongozo wa busara na kunitia moyo wakati nilipohitaji. Kwa muda wote ambao Rosalynn alikuwa duniani, siku zote nilijua ni mtu aliyenipenda na kuniunga mkono.

Mke huyo wa rais wa zamani alikiri katika mahojiano na VOA mwaka 2014 kwamba siri ya ndoa yake iliyo ndefu na Jimmy Carter ilikuwa kupeana nafasi na heshima. Rais Joe Biden ametoa salamu za rambi rambi kwa familia ya Cater.

VOA
+ posts