Home Michezo Ronald Koeman atupia Barcelona lawama kisa De Jong

Ronald Koeman atupia Barcelona lawama kisa De Jong

Kocha wa Uholanzi Ronald Koeman ameilaumu klabu ya Barcelona kwa kushindwa kudhibiti jeraha la kiungo Frenkie De Jong.

0
Kocha wa Uholanzi Ronaldo Koeman
kra

Kocha wa zamani wa Barcelona Ronald Koeman ameilaumu klabu ya Barcelona kwa jeraha la kiungo wa Uholanzi Frenkie de Jong ambalo limemfanya kukosa kushiriki michuano ya Euro itakayoanza siku ya Ijumaa 15, 2024 wiki hii huko Ujerumani.

Frenkie De Jong 27, alitemwa kwenye kikosi cha Uholanzi kitakachoshiriki michuano ya Euro 2024 siku ya Jumatatu, kutokana na tatizo la kifundo cha mguu, jeraha ambalo limemsumbua kwa muda.

kra

Mholanzi huyo amekuwa akisumbuliwa na jeraha la kifundo cha mguu tangu Septemba mwaka jana na kumlazimu kusalia nje zaidi ya mechi 20 za Barcelona kwenye msimu uliopita.

Frenkie De Jong hatoshiriki michuano ya Euro 2024 na Uholanzi kutokana na jeraha la kifundo

Baada ya Uchunguzi uliofanywa na madaktari wa timu ya Uholanzi pamoja na kocha, iliamuliwa kwamba De Jong hayuko sawa vya kutosha kushiriki michezo wiki zijazo.

Kocha wa Uholanzi Ronald Koeman sasa ameitupia lawama klabu ya Barcelona kwa janga hili ambalo limempata Mchezaji wake.

Akiongea na wanahabari baada ya taarifa za kujiondoa kwa De Jong kwenye kambi ya Uholanzi kuthibitishwa, Koeman alisema: “Tumezingatia kwamba Frenkie de Jong hatakuwa amepona kwenye wiki tatu zijazo. Alikuwa na historia na jeraha hili kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia na haifai kumuhatarisha. Klabu yake ilimuhatarisha hapo awali na sasa lazima sisi tuilipie”

Msimu huu Frenkie de Jong ametatizwa mno na majeraha, zaidi ya hapo awali. De Jong amepatwa na matatizo matatu ya kifundo cha mguu ambayo yamemmfanya kukosa jumla ya michuano 27 kati ya 53 kwenye ngazi ya klabu.

francis ngala
Website | + posts

I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.