Home Michezo Rising Starlets yarejea nyumbani baada ya kuishinda Angola mechi ya kufuzu Kombe...

Rising Starlets yarejea nyumbani baada ya kuishinda Angola mechi ya kufuzu Kombe la Dunia

0

Timu ya taifa ya akina dada wasiozidi  umri wamiaka 20 Rising Starlets, iliwasili nchini mapema Jumatatu kutoka Luanda, Angola ilikofuzu kwa raundi ya tatu  ya mechi za kuwania tiketi kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Colombia.

Starlets walisajili ushindi wa mabao manne kwa bila katika mchuano wa marudio na kufuzu kwa raundi ya tatu kwa ushindi wa jumla wa mabao 10 kwa moja kufuatia ushindi wa amabao 6-1 katika duru ya kwanza jijini Nairobi.

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko ameituza timu hiyo shilingi laki mbili kwa ushindi huo.

Kenya imeratibiwa kumenyana na Cameroon katika raundi ya tatu huku mshindi akichuana na mshindi kati ya Misri na Congo katika raundi ya nne na ya mwisho.