Home Michezo Risala za rambirambi zamiminika kufuatia kifo cha Kiptum

Risala za rambirambi zamiminika kufuatia kifo cha Kiptum

0

Viongozi mbalimbali wanazidi kutuma risala za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa mwenda zake mshikilizi wa rekodi ya dunia ya marathon kelvin Kiptum.

Rais William Ruto amemtaja kuwa miongoni mwa wanaspoti bora duniani na mwenye heshima ya kipekee na ambaye alijizatiti na kuvunja rekodi ya dunia akiwa na umri mdogo wa miaka 24.

Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, amesema kuwa amehuzunishwa na kifo cha Kiptum na kuungana wa wakenya wengine kumwomboleza nyota huyo ambaye alipeperusha bendera ya Kenya na kuleta sifa tele nchini.

Naye Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amesema kuwa Kiptum alikuwa mwenye talanta ya kipekee na kujitolea kwake katika riadha kumewavutia watu wengi kujiunga na riadha.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amemtaja kiptum kuwa shujaa ambaye taifa zima linaomboleza.

Kiongozi wa chama cha wiper Kalonzo Musyoka amemsifu Kiptum kuwa barurubaru aliyekuwa anakuwa kwa kasi zaidi nchini na hata duniani katika fani ya riadha.

Bingwa mara mbili wa mbio za nyika za Olimpiki Eliud Kipchoge amemsifu kuwa mwanariadha ambaye angefanikiwa zaidi siku za usoni.

Rais wa shirikisho la Riadha Ulimwenguni Seb Coe pia ametaja kupokea kifo cha Kiptum kwa masikitiko makubwa.

Boniface Musotsi
+ posts