Chama cha Riadha Kenya kimewataka wanariadha kujisali kwa wingi kushiuriki mkondo wa pili wa mashindano ya uwanjani maarufu kama Track and Field Weeekend Meet, utakaoandaliwa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex kaunti ya Nairobi baina ya Januari 5 na 6 mwaka ujao.
AK imesema kuwa mashindano hayo hatakuwa ya wazi kwa wanariadha wote watakaojiandikisha, huku washiriki wakihitaji kuchukua kuchukua nambari za usajili binafsi tarehe 4 mwezi ujao.
Mashindano hayo yatakuwa ya kwanza mwaka ujao ambao michezo ya Olimpiki inatarajiwa kuandaliwa kati ya mwezi Julai na Agosti jijini Paris Ufaransa.