Rais William Ruto amemteua Renson Mulele Ingonga kuwa Mkurugenzi mkuu mpya wa mashtaka ya umma kumrithi Noordin Haji, aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa huduma ya Ujasusi NIS.
Tayari Ruto amewasilisha jina la Igonga Bungeni ili kusailiwa.
Rais Ruto amemteua Igonga kutoka kwa orodha ya watu 15 waliosajiliwa na tume ya kuwaajiri watumishi wa umma.
Hajiali alihudumu katika afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma tangu Agosti mwaka 2018.
Hadi uteuzi wake Ingonga amekuwa naibu Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.
Wengine waliokuwa wameorodheshwa na tume ya kuwaajiri wafanyikazi wa umma kwa kazi hiyo ni Kamishna wa zamani wa tume ya IEBC Thomas Letangule, Francis Andayi, wakili Danstan Omari, Taib Ali, Jacinta Nyamosi, Victor Mule , Tabitha Ouya ,David Ruto, Winston Ngaira, Peter Mailanyi, Lilian Okumu, Jacob Ondari, James Ndegwa,na d David Okachi