Shirika la Msalaba Mwekundu lilitoa msaada wa vyakula na bidhaa nyinginezo za matumizi kwa wakazi wa eneo la Elwak kaunti ya Mandera,walioathiriwa kutokana na mafuriko.
Jumla ya familia 700 zilinufaika kwa msaada huo wa Jumatano, uliongozwa na Gavana wa Mandera Mohammed Khalif ,Balozi wa Uingereza nchini Kenya Neil Wigan,Mbunge wa Mandera Kusini,na maafisa kutoka kwa shirika la Masalaba Mwekundu .
Familia 23,279 zimeathiriwa kwa mafuriko katika kaunti ya Mandera, ikiwa kaunti ya tatu iliyoathirika vibaya kwa mafuriko nchini baada ya Tana River na Garissa.