Ratiba ya timu 16 bora zitakazoshiriki awamu ya mwondoano ya kipute cha bara Ulaya nchini Ujerumani imekamilika baada ya mechi za makundi .
Uswizi itafungua awamu hiyo jumamosi dhidi ya mabingwa watetezi Italia ugani Olympiastadion Berlin, kabla ya wenyeji Ujerumani kuzichapa dhidi ya Denmark uwanjani Signal Iduna Park katika mechi ya pili.
Jumapili Uingereza itakabana koo na Slovakia uwanjani Veltins Juni 30 saa moja usiku kabla ya Uhispania kugaragazana na Georgia .
Ufaransa itachuana na Ubeligiji Julai mosi nao Ureno wapimane nguvu na Slovenia ugani Deutsche Bank Park Julai .
Romania itamenyana na Uholanzi kiwarani Allianz Arena tarehe mbili Julai saa moja usiku kisha Austria itoane jasho na Uturuki ugani Red Bull Arena Leipzig katika mechi ya mwisho.