Ratiba ya mechi za robo fainali kuwania kombe la AFCON, imebainika kufuatia kukamilika kwa mechi za awamu ya 16 bora .
Nigeria Super Eagles watafungua ratiba dhidi ya Palancas Negras kutoka Angola Ijumaa Februari 2, kabla ya DR
Congo maarufu kama Leopards kukabiliana na Syli National ya Guinea.
Jumamosi Februari 3, Mali ukipenda The Eagles watashuka dimbani dhidi ya wenyeji Ivory Coast maarufu kama Elephants na Afrika Kusini,Bafana Bafana wafunge ratiba ya dhidi ya Cape Verde wanaojulikana kama Blue Sharks.
Timu 16 zimeyaaga mashindano hayo huku nane pekee zikisalia.