Home Michezo Rapinoe astaafu soka ya kimataifa

Rapinoe astaafu soka ya kimataifa

Rapinoe, 38, aliichezea Marekani kwa mara ya kwanza mwaka 2006 na hadi kustaafu alikuwa amepiga mechi 203 za kimataifa akipachika magoli 63 na kutwaa kombe la dunia mara mbili mwaka 2015 na 2019.

0

Mchezaji wa timu ya taifa ya Marekani Megan Rapinoe amestaafu rasmi kutoka soka ya kimataifa.

Rapinoe aliye na umri wa miaka 38 alicheza mchuano wa mwisho katika ushindi wa Marekani wa mabao 2 kwa bila dhidi ya Afrika Kusini mapema Jumatatu mjini Chicago.

Rapinoe, 38, aliichezea Marekani kwa mara ya kwanza mwaka 2006 na hadi kustaafu kwake, alikuwa amepiga mechi 203 za kimataifa akipachika magoli 63 na kutwaa kombe la dunia mara mbili mwaka 2015 na 2019.

Mwanandinga huyo anatarajiwa kugura soka ya kulipwa Oktoba 15 atakapoichezea klabu yake ya Chicago Red Stars.

Website | + posts