Home Habari Kuu Rais William Ruto awasili Guinea Bissau kwa ziara rasmi ya kiserikali

Rais William Ruto awasili Guinea Bissau kwa ziara rasmi ya kiserikali

0
Rais William Ruto awasili nchini Guinea-Bissau.

Rais William Ruto leo Alhamizi amewasili nchini Guinea Bissau, baada ya kukamilisha ziara rasmi nchini Ghana.

Kulingana na taarifa kutoka kwa hatibu wa ikulu Hussein Mohamed, akiwa nchini Guinea-Bissau, Rais Ruto ananuia kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kutambua mbinu mpya za ushirikiano na kampuni ya Lusophone Africa chini ya mkataba wa eneo huru la kibiashara barani Afrika.

Hii inajumuisha kuimarisha ushiriki wa sekta ya kibinafsi katika kilimo, utengenezaji bidhaa na ubadilishanaji teknolojia miongoni mwa sekta nyingine.

Akiwa nchini Ghana, Rais Ruto alishuhudiwa kutiwa saini kwa mikataba saba ya maelewano, MOU kati ya Kenya na Ghana kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Website | + posts