Home Habari Kuu Hampati ng’oo! Rais Ruto asisitiza hakuna serikali ya ‘nusu mkate’

Hampati ng’oo! Rais Ruto asisitiza hakuna serikali ya ‘nusu mkate’

Rais William Ruto amepuzilia mbali uwezekano wa makubaliano ya kugawana serikali na upinzani huku akisema vitisho vya upande wa Upinzani haviwezi kubadilisha fikra zake.

0

Rais William Ruto amepuuzilia mbali uwezekano wa makubaliano ya kugawana serikali na upinzani huku akisema vitisho vya upande wa upinzani haviwezi kubadilisha fikra zake.

Aidha Rais Ruto ameuonya upinzani dhidi ya machafuko na uchochezi wa umma ambao umeendelea kukwamisha na kudhuru biashara za Wakenya.

“Tumewaambia (AZIMIO) ile vitisho walikuwa nayo ili ati ndio wapate serikali nusu mkate haitafanyika tena, haiwezekani. Na hawa watu nitawakalia ngumu,” alisema Ruto.

Akiongea Agosti 5, eneo la Githurai kaunti ya Kiambu, ambapo ameanza rasmi ziara ya maendeleo katika eneo la Mlima Kenya, Rais Ruto amesema viongozi wanaolipa vijana kuzua fujo na kuharibu biashara za wengine hawataruhusiwa kufanya hivyo.

“Hakuna mtu awe mrefu au mfupi, wa chama hiki au kile ataendesha mambo ya vita katika taifa letu la Kenya. Ati viongozi wanatoa pesa kulipa vijana wapigane, waharibu mali, waharibu biashara ya watu, hiyo haitafanyika tena.”

Rais William Ruto akihutubia umma eneo la Githurai, kaunti ya Kiambu

Wakati huo huo, Rais Ruto ametoa ahadi ya kujenga masoko mengine kumi na tano mapya katika eneo la Githurai ambayo yatakuwa miongoni mwa masoko 400 ambayo ameahidi kujenga katika kipindi cha miaka mitatu.

“Hapa Kiambu tutawajengea masoko mengine kumi na tano kwa sababu mimi nilikubaliana na kina mama mboga ya kwamba kazi ni kazi.”

 

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here