Home Kimataifa Rais wa Uganda kuhudhuria kongamano la ushirikiano wa Urusi na Afrika

Rais wa Uganda kuhudhuria kongamano la ushirikiano wa Urusi na Afrika

0

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameondoka nchini humo kuelekea Urusi kuungana na viongozi wengine wa bara Afrika kwa awamu ya pili ya kongamano kuhusu uchumi na usaidizi wa kibinadamu kati ya Urusi na Afrika.

Aliagwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Entebbe na Waziri katika Afisi ya Rais Babirye Milly Babalanda, Mkuu wa Utumishi wa Ummma na Katibu wa Baraza la Mawaziri Lucy Nakyobe Mbonye na Mkuu wa Majeshi Wilson Mbasu Mbadi miongoni mwa wengine.

Awamu hiyo ya pili ya kongamano la chumi na usaidizi wa kibinadamu kati ya Russia na Afrika, ulistahili kuandaliwa jijini Addis Ababa nchini Ethopia Oktoba, 2022 lakini ukaahirishwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin Julai, 2022 labda kutokana na hatua ya Urusi ya kuvamia Ukraine.

Akiwa Urusi, Rais Museveni anatarajiwa kufanya mazungumzo ya faragha na rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu masuala kadhaa.

Ataandaa mikutano ya pande mbili pia na jumbe kutoka nchi mbali mbali kando kando ya kongamano hilo.

Kongamano hilo ambalo litafanyika jijini St. Petersburg litaandaliwa Alhamisi na Ijumaa na baadaye Museveni ataelekea jijini Belgrade nchini Serbia kuzindua kituo cha kutangaza utalii, fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana nchini Uganda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here