Home Habari Kuu Rais wa Poland azuru taasisi ya mafunzo ya wazima moto Kiambu

Rais wa Poland azuru taasisi ya mafunzo ya wazima moto Kiambu

0

Rais wa Poland Andrzej Duda, alikamilisha ziara yake hapa nchini kwa kuzuru kituo cha kutoa mafunzo kwa wazima moto kaunti ya Kiambu.

Rais huyo akiwa ameandamana na mke wake Agata Kornhauser- Duda, walikaribishwa na Gavana wa kaunti ya Kiambu Kimani wa Matangi.

Wakati wa ziara hiyo, wanafunzi wanaosomea taaluma ya kukabilana na moto na dharura zingine, walionyesha utaalam mbali mbali uliojumuisha kuzima moto, kushughulikia ajali za barabarani, utoaji wa huduma ya kwanza pamoja na gari la kuzima moto ambalo ni la kwanza kuundiwa hapa nchini kwa ufadhili wa serikali ya Poland mwaka 2021.

Gavana wa kaunti hiyo Kimani Wamatangi, aliwatuza vyeti wanafunzi ha ambao walikamilisha mafunzo yao na sasa wanasubiri kupelekwa katika maeneo mbali mbali katika kaunti hiyo.

Taasisi ya mafunzo ya wazima moto ya Kiambu, ni miongoni mwa taasisi kuu hapa nchini ambazo  hutoa mafunzo ya kitaalam kuhusu uokoaji na kukabiliana na mito.

Taasisi hiyo ilijengwa na serikali kwa usaidizi wa shirika la kutoa misaada la Poland (PCIA), na kilifunguliwa 2021.

Serikali ya Poland pia ilitoa vifaa vya kujikinga kwa taasisi hiyo

Rais huyo ambaye amekuwa kwa ziara rasmi ya wiki moja  barani Afrika, atazuru Rwanda na Tanzania.