Home Kimataifa Rais wa Malawi Lazarus Chakwera akosolewa

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera akosolewa

0

Wanasiasa wa upinzani nchini Malawi na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamemkosoa Rais Lazarus Chakwera na serikali yake kwa kutuma vijana 221 wa Malawi kufanya kazi katika mashamba nchini Israel.

Hatua hiyo ya Jumamosi ilifuatia msaada wa Israel wa $60m (£47m) wiki mbili zilizopita kusaidia kuimarisha uchumi wa Malawi.

Mpango huo wa mauzo ya nje ya nchi umekosolewa huku kukiwa na wasiwasi juu ya usiri ambao ulifanyika na hatari zinazowezekana kwa raia wakati ambapo Israeli iko kwenye mzozo na kundi la Hamas la Palestina.

“Kutuma watu katika nchi inayokumbwa na vita kama Israel, ambako baadhi ya nchi zinaondoa raia wake ni jambo ambalo halijasikika,” kiongozi wa upinzani wa Malawi Kondwani Nankhumwa aliambia kipindi cha Newsday cha BBC.

Pia alihoji ni kwa nini serikali iliweka mpango huo kuwa siri, na kuliarifu bunge tu kuhusu mpango wa kutuma wafanyikazi katika nchi ambayo haikutajwa tarehe 22 Novemba.

Serikali imetetea mpango huo, ikisema kuwa itasafirisha Wamalawi kwenda Israel na nchi nyingine “kutimiza ahadi ya utawala huu wa kubuni nafasi za kazi na kuwawezesha vijana”.

BBC
+ posts