Rais Abdulmadjid Tebboune ameshinda muhula wa pili kuliongoza taifa la Ageria, baada ya kupata asilimia 95 ya kura zilizopigwa Jumamosi iliyopita.
Matokeo hayo yalitangazwa Jumapili na kuondoa uwezekano wa kuwa na duru ya pili ya uchaguzi.
Mpinzani wake mkuu amelalamikia kuhusu kuwepo kwa visa vingi vya wizi wa kura.
Wapinzani wakuu Abdelaali Hassani Cherif alipata asilimia 3 naye Youcef Aouchiche akapata asilimia 2.
Idadi ya waliopiga kura ilikuwa asilimia 48 ya wapiga kura waliosajiliwa.
Tebboune alichaguliwa kwa muhula wa kwanza mwaka 2019 kufuatia mapinduzi yaliyomng’atua mamlakani Abdulaziz Bouteflika, aliyekuwa mamlakani kwa kipindi cha miaka 20.