Home Habari Kuu Rais Suluhu awasili Indonesia kwa ziara ya siku tatu

Rais Suluhu awasili Indonesia kwa ziara ya siku tatu

0
kra

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amewasili nchini Indonesia kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu. 

Anasema ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Rais wa Indonesia Joko Widodo.

kra

Tanzania na Indonesia zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia ambao umedumu kwa kipindi cha miaka 59 sasa.

“Uhusiano wa Tanzania na Indonesia ambao mapema mwezi huu (Januari 13) ulitimiza miaka 59, umekuwa wenye tija kwa nchi yetu na mamilioni ya Watanzania hasa kwenye kilimo na biashara,” amesema Rais Suluhu. 

“Tunaendelea kuifanya kazi ya kukuza uhusiano huu ili kuleta tija zaidi kiuchumi kwa nchi yetu.”