Home Kimataifa Rais Samia apongeza Daktari aliyetuzwa na chuo cha Havard

Rais Samia apongeza Daktari aliyetuzwa na chuo cha Havard

0
kra

Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amempongeza Daktari Karim Manji ambaye ni profesa katika masuala ya tiba ya watoto na vijana.

Hii ni baada ya Profesa huyo kutunukiwa tuzo ya mwanafunzi bora wa awali na taasisi ya T.H Chan ya mafunzo ya afya ya umma ya chuo cha Harvard.

kra

Rais alitumia mitandao ya kijamii ambapo alichapisha picha ya Daktari huyo na kuandika, “Pongezi za dhati kwa Profesa Karim Manji, bingwa, mkufunzi na mtafiti katika eneo la tiba ya watoto na afya ya vijana, kwa ushindi wa tuzo ya Alumni Award of Merit toka Shule ya Afya ya Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard T.H. Chan School of Public Health).”

Aliemdelea kummiminia sifa akisema kwamba kwa zaidi ya miaka 30, Profesa Manji amekuwa daktari, mkufunzi na mtumishi wa kupigiwa mfano katika Hospitali ya Taifa na Chuo Kikuu cha Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili.

“Tunajivunia kujitoa kwako kwa nchi yetu, utafiti, ushauri, utumishi na malezi yako kwa mamia ya wanafunzi ambao sasa ni madaktari katika eneo hili muhimu la afya kwa nchi yetu.” alimalizia kiongozi huyo wa Tanzania.

Manji ndiye raia wa kwanza wa Tanzania kuwahi kutunukiwa tuzo hiyo ya hadhi ya juu na atapokezwa tasmi Septemba 27, 2024 huko Boston nchini Marekani.

Tuzo hiyo hutolewa kwa wanafunzi wa zamani wa taasisi hiyo wanaobainika kutoa mchango faafu kwa afya ya umma.

Website | + posts