Home Kimataifa Rais Samia aagiza Hanang kusafishwe kufikia usiku leo

Rais Samia aagiza Hanang kusafishwe kufikia usiku leo

0
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameelekeza maafisa wanaotekeleza shughuli za uokoaji na urejesho wa wilaya ya Hanang baada ya mafuriki wahakikishe wamemaliza kazi hiyo kufikia usiku wa leo.

Anataka mji wa Katesh na maeneo ya karibu yaondolewe mchanga, miti, mawe na uchafu mwingine ulioachwa na maji ya mafuriki ili wakazi wa eneo hilo warejelee shughuli za kawaida.

Ujumbe huo wa Rais Samia uliwasilishwa na waziri wa ujenzi, Innocent Bashungwa ambaye ameelezea pia kwamba kazi kubwa inayoendelea sasa ni uondoaji wa matope.

Waziri huyo yuko katika eneo hilo ambapo anakagua kazi inayoendelea akiwa na mwenzake wa afisi ya Waziri Mkuu Jenista J. Mhagama, waziri wa madini Antony Mavunde, Naibu Waziri wa TAMISEMI Dkt. Festo Dugange na wengine

Wilaya ya Hanang ambayo inapatikana katika mkoa wa Manyara nchini Tanzania ilikumbwa na mafuriko mabaya ambayo yalisababisha vifo na uharibifu mkubwa wa mali.

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko Hanang ni zaidi ya watu 60.

Website | + posts