Home Kimataifa Rais Samia aadhimisha miaka 24 tangu kifo cha Nyerere

Rais Samia aadhimisha miaka 24 tangu kifo cha Nyerere

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, siku ya Jumamosi amehudhuria Misa Maalum ya kumuombea mwanzilishi wa taifa hilo, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,katika Parokia ya Roho Mtakatifu, Babati Mjini, Jimbo Katoliki la Mbulu.

Ibada hiyo iliadhimisha miaka 24 tangu kufariki kwa Nyerere.

Kwenye hotuba yake Rais Samia amemsifia kuwa kiongozi shupavu,mahiri akiongeza kuwa wanajivuni misingi aliyojengea, inayoendelea kuunganisha taifa hilo na kuwa na mshikamano.

Website | + posts