Home Habari Kuu Rais Ruto:Upatanishi ni nguzo muhimu katika mchakato wa upatinishi Sudan Kusini

Rais Ruto:Upatanishi ni nguzo muhimu katika mchakato wa upatinishi Sudan Kusini

Rais alisema Kenya iko tayari kusaidia  kumaliza mizozo na ukosefu wa utulivu nchini Sudan ili kufikia amani na ustawi ambao watu wake wamepigania kwa muda mrefu.

0

Rais William Ruto ametoa wito wa kujitolea kwa dhati kwa pande zote zinazohusika katika mchakato wa amani wa Sudan Kusini ili kufikia amani ya kudumu.

Akizungumza  aliposhuhudia uzinduzi wa Mchakato wa Upatanishi wa Sudan Kusini unaoongozwa na Kamanda wa zamani wa Jeshi Lazarus Sumbeiywo, katika Ikulu ya Nairobi, kiongozi wa taifa alisema mchakato wa upatanishi unalenga  kumaliza migogoro na ukosefu wa utulivu wa kisiasa nchini Sudan Kusini.

Alisema Mkakati wa Tumaini, ambao ni mpango wa upatanishi wa ngazi ya juu huko Sudan Kusini, umeleta pamoja makundi manane ya vyama na makundi na kuhakikisha mchakato huo unakuwa jumuishi na unafanyika nyumbani.

Rais alisema Kenya iko tayari kusaidia  kumaliza mizozo na ukosefu wa utulivu nchini Sudan ili kufikia amani na ustawi ambao watu wake wamepigania kwa muda mrefu.

“Natoa ahadi ya kuunga mkono mchakato huo na katika kila hatua ya majadiliano hayo,” alisema Rais Ruto.

Kwa upande wake Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alimshukuru Rais Ruto kwa kukubali jukumu la kusuluhisha mzozo nchini  Sudan Kusini. Rais Kiir alisema serikali ya Sudan Kusini itajadiliana kwa nia njema na kwa nia iliyo wazi.

Sumbeiywo aliwapongeza washirika wa kikanda na kimataifa kwa kuunga mkono mchakato wa amani nchini Sudan kusini.

Alisema, kwa mwezi mmoja uliopita, mkakati huo wa upatanisho umefanya ushauri mpana  na pande zinazohusika ili kuhakikisha mchakato huo unakuwa jumuishi.