Home Habari Kuu Rais Ruto: Uchumi wa Kenya umeimarika

Rais Ruto: Uchumi wa Kenya umeimarika

0

Rais William Ruto ametetea utendekazi wake akisema uchumi wa nchi umeimarika licha ya shinikizo kutoka kwa Wakenya kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha.

Rais Ruto amesema haya Jumapili jioni katika kikao na wanahabari katika Ikulu ya Nairobi.

Amesema tayari serikali yake imedhibiti madeni yake yaliyokuwa yakiiponza nchi.

Hata hivyo, Rais amesema itawabidi Wakenya kuwa na subira kabla ya hali kutengemaa.