Home Kimataifa Rais Ruto: Sitazindua ujenzi wa barabara mpya

Rais Ruto: Sitazindua ujenzi wa barabara mpya

Rais alisema anapokea shinikizo za kuanzisha ujenzi wa barabara mpya, lakini alisisitiza kuwa atakamalisha zile ambazo zinajengwa kwanza, bila kujali waanzilishi wa miradi hiyo.

0
Rais Ruto ajibu maswali ya wananchi kaunti ya Kisumu.
kra

Rais William Ruto, amesema serikali yake haitaanzisha ujezi wa barabara mpya, hadi ujenzi wa barabara zilizokwama utakapokamilika.

Akijibu maswali kutoka kwa wananchi katika kaunti ya Kisumu, Rais alisema anapokea shinikizo za kuanzisha ujenzi wa barabara mpya, lakini alisisitiza kuwa atakamalisha zile ambazo zinajengwa kwanza, bila kujali waanzilishi wa miradi hiyo.

kra

“Nilikuwa katika eneo hili kufufua ujenzi wa barabara ambao ulikuwa umekwama. Nawahakikishia kuwa ujenzi wowote wa barabara uliokuwa umekwama, utakamlishwa. Hatutaanza ujenzi wa barabara mpya, hadi tukamilishe zile ambazo zilikuwa zimekwama,” alisema Rais Ruto.

Rais alisema hatatia sahihi yake kwa ujenzi mpya wa barabara, akisema lengo lake kuu ni kuhakikisha barabara zilizoanzishwa awali zinakamilika.

“Sina haja ya kuwa na sahihi zangu katika barabara hizo, nina haja ya kuona ujenzi wa barabara ulioanzishwa awali, unakamilika,” alodokeza Rais Ruto.

Katika ziara yake leo Alhamisi katika kaunti ya Homa Bay, Rais alizindua miradi kadhaa ya maendeleo katika eneo hilo, na pia aliungana na wakazi wa Magunga- Suba Kusini katika kaunti ya Homabay kwa ibada ya shukrani ya waziri wa fedha na mipango ya uchumi John Mbadi.

Website | + posts